Kongamano la maonesho ya kilimo SUA kuanza tarehe 4 hadi 6 December 2019

Litaunganisha wadau wa kilimo kuelekea Tanzania ya Viwanda

Na Vedasto George

Ndaki ya Kilimo katika Chuo Kikuu cha Sokoine Cha Kilimo SUA kwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini wameandaa kongamano la siku tatu la maonesho ya kilimo na mifugo litakaloanza tarehe 4 hadi 6 december, 2019 lengo likiwa ni kujadili changamoto na kutambua fursa zilizopo katika sekta hiyo kuelekea Tanzania ya Viwanda.

Prof. Maulid Mwatawala akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani kuelezea Kongamano la maonesho ya kilimo (Picha na Gerald Lwomile)

Akizungumza na vyombo vya habari Rasi wa Ndaki hiyo Prof. Maulid Mwatawala amesema kogamano hilo litawakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wakulima na wafugaji wakubwa kwa wadogo,watafiti, maafisa ugani na wadau wengine mbalimbali

Amesema kuwa SUA kama chuo pekee cha kilimo nchini pamoja na kuwa na majukumu mengine kama kufundisha lakini pia kinayo nafasi ya kutoa elimu inayohusu kilimo ili kuwawezesha wakulima na wafugaji kujifunza mbinu bora za kilimo na ufugaji

Aidha Prof. Mwatawala amebainisha kuwa kongamano hilo litawasaidia wakulima na wafugaji  kuelewa  na kutambua jinsi gani wanaweza kuwekeza katika sekta hizo za kilimo na mifugo na jinsi wanavyoweza kupata mikopo ya riba nafuu kutoka kwenye taasisi za mikopo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya maonesho hayo Prof. Sebasitian Chanyambuga amesema kuwa katika kongamano hilo kutakuwa na makampuni yanayozalisha mbegu za kilimo na kuongeza kuwa ndaki ya kilimo imekuwa ikifanya kongamano hilo kila mwaka.

Prof. Chenyambuga akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani kuelezea Kongamano la maonesho ya kilimo (Picha na Gerald Lwomile)

Kongamano hilo kwa mwaku huu limebeba ujumbe usemao “Kuelekea Tanzania ya viwanda  na uchumi wa kati, jukumu na michango ya wadau wa sekta za kilimo na mifugo”

Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakisikiliza mkutano kati yao na Rasi wa Ndaki ya Kilimo SUA (Picha na Gerald Lwomile)

Related Posts

Next Post

Discussion about this post

RECOMMENDED