Komputa 21 kati 23 zilizoibwa shule ya msingi Msamvu B zikamatwa

Mlinzi atokomea kuzikojulikana

Kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro Willbroad Mutafungwa akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani (Picha na Vedasto George)

Na Vedasto George, Morogoro

Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro limekamata komputa 21 kati ya 23 zilizokuwa zimeibwa shule ya msingi Msamvu B ambazo zililetwa shuleni hapo kwa ajili ya kufundishia wanafunzi

Akizungumza na Wanahabari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro  Willbroad Mutafungwa amesema watuhumiwa watatu tayari wamekamatwa na kufanyiwa mahojiano  ambapo wamekiri kuhusika katika tukio hilo huku mlizi wa shule hiyo akiwa ametokomea kusikojulikana

“Lakini katika hali ya kushangaza tukapata taarifa kuwa mlinzi aliyekuwa amekabidhiwa dhamana ya kuwa mlinzi katika shule hiyo na mali zingine za shule hiyo ametoweka na wezi badala ya kulinda” amesema Mutafungwa

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Msamvu Bw. Elidad Methew amelishukuru Jeshi la polisi kwa kufanya kazi yake kwa weledi mkubwa na kuelezea namna komputa hizo zilivyokuwa zinatumiwa, huku baadhi ya wanafunzi wakieleza furaha yao mara baada ya kukamatwa kwa komputa hizo

Katika tukio jingine Kamanda Mutafungwa amesema kwa kushirikiana na askari wa wanyamapori wamemkamata mtu mmoja akiwa na pembe moja ya ndovu yenye uzito wa kilogramu 3  ambayo ilikuwa ikisafirishwa kwa kutumia pikipiki  yenye namba za usajiri MC 818 BTU.

 

Related Posts

Next Post

Discussion about this post

RECOMMENDED