Kamati ya Kuthibiti Uadilifu SUA yajipanga kusimamia uadilifu

Kuthibiti matendo ya rushwa na uonevu

Na Gerald Lwomile

SUA

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA, kimewataka wanafunzi, wafanyakazi na wanajumuiya wa SUA kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa Kamati ya Kuthibiti Uadilifu KKU iliyopo SUA ili kuhakikisha kila mwanafunzi na mfanyakazi katika taasisi hiyo anawajibika kwa kufanya kazi kwa uadilifu, kuepuka rushwa na matendo mbalimbali ya uonevu

Hayo yamesemwa Februari 15, 2020 na Naibu wa Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Utawala na Fedha, Prof. Yasinta Muzanila wakati akifungua mafunzo kuhusu Kamati ya Kuthibiti Uadilifu kwa viongozi mbalimbali wa Serikali ya wanafunzi SUASO na wawakilishi wa madarasa iliyofanyika chuoni hapo

Naibu wa Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Utawala na Fedha, Prof. Yasinta Muzanila akisisitiza kuhusu uadilifu ( Picha na Mabula Mussa)

“Serikali yetu hii ya awamu ya 5 inayo mikakati mingi ya kuboresha utawala bora na mkakati mmoja wapo ni kuthibiti uadilifu pia kuthibiti rushwa, na kama tunavyofamu kwamba rushwa ni adui wa haki na si kwa Tanzania tu bali Ulimwengu mzima” amesema Prof. Muzanila

Naye Mwenyekiti wa KKU chuoni hapo Prof. Christopher Mahonge amesema kamati imeandaa mpango kazi wa mapambano dhidi ya rushwa, kupokea, kuchambua na kushughulikia malalamiko toka ndani na nje yanayotokana na ukiukwaji wa maadili

“Lakini pia kamati itashiriki katika kutoa mafunzo kuhusu maadili, utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa kwa maafisa wa ngazi za kati, mameneja na watumishi wa kawaida” amesema Prof. Mahonge

Mwenyekiti wa KKU chuoni hapo Prof. Christopher Mahonge akionyesha moja ya chombo cha kutolea maoni (Picha na Mabula Mussa)

Prof. Mahonge ameongeza kuwa taasisi za serikali ikiwemo SUA zinao wajibu mkubwa wa kuhakikisha zinatoa huduma bora na kuzingatia masilahi ya umma na thamani ya fedha inayotumika katika huduma hizo hivyo ni muhimu kwa kila mtu kuwajibika

Akizungumzia mafunzo hayo Rais wa Serikali ya Wanafunzi SUA Bw. Mbalamwezi Hussein Ismail amesema hivi sasa suala la uadilifu limekuwa changamoto kubwa kwa watanzania kwa hiyo mpango huu wa Serikali utawaweka watu kuwa na ufahamu juu ya masuala ya rushwa na uonevu

Naibu wa Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Utawala na Fedha, Prof. Yasinta Muzanila aliyekaa katikati akiwa na viongozi wa Serikali ya wanafunzi kushoto waliokaa ni M/Kiti wa KKU Prof. Mahonge anayefuatia kutoka Prof. Mahonge ni Mshauri wa wanafunzi SUA Bw. Pure na kushoto wa pili ni Rais wa SUASO Bw. Mbalamwezi na kwanza kushoto ni Waziri Mkuu SUASO Bi. Tairo

Naye Waziri Mkuu wa Serikali ya wanafunzi SUA Bi. Jenipher Karoli Tairo amesema jambo hili litasidia wanafunzi kusoma katika mazingira rafiki ambayo yatawasaidia katika masomo yao

“Uadilifu unaposimamiwa katika mazingira ya shule hakika wanafunzi watasoma katika mazingira ambayo ni rafiki kwa maana ninaamini hakutakuwa na bugudha kutoka kwa waalimu hususani kwa wanafunzi wa kike” amesema Jenipher

Wajumbe wa kamati ya KKU wakiwa na Mgeni rasmi Naibu wa Makamu wa Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha Prof. Yasinta Muzanila na Viongozi wa SUASO (Picha na Mabula Mussa)

Fuatilia Katika video

Source: SUAMEDIA
Via: SUAMEDIA

Related Posts

Next Post

Discussion about this post

RECOMMENDED