Na:Gerald Lwomile Wakati Maonesho ya Nanenane yanatarajiwa kuanza rasmi kesho Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kimesema kiko tayari kuonesha Teknolojia mpya na tafiti mbalimbali kupitia Maonesho hayo 2018 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Prof. Raphael Chibunda akipokea maelezo kuhusu maonesho ya Nanenane toka kwa Prof. Mwatawala siku moja kabla ya kuanza kwa Maonesho hayo wakati alipotembelea mabanda ya SUA.(Picha na Gerald Lwomile).
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda amewahakikishia wakulima na wananchi kwa ujumla watakaofika kwenye maonesho hayo kuwa watapata fursa ya kuongea na wataalamu wa kilimo kwa minajili ya kufanya kilimo chenye tija.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Prof. Raphael Chibunda akiangalia vipando katika maonesho ya Nanenane siku moja kabla ya kuanza kwa Maonesho hayo wakati alipotembelea mabanda ya SUA.(Picha na Gerald Lwomile).
Aidha kupitia maonesho hayo Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kitafanya udahili wa moja kwa moja kwa wanafunzi wanaotaka kusoma masomo ya sayansi pamoja na masomo mengine yatolewayo na chuo hicho.
Maonesho ya Nanenane ya mwaka 2018 yamebebwa na kauli mbiu isemayo “WEKEZA KATIKA KILIMO MIFUGO NA UVUVI KWA MAENDELEO YA VIWANDA”. |