Na Calvin Gwabara Waziri wa Nishati na Madini Mh. Angellah Kairuki amewataka maafisa waandamizi wa Tume ya Madini nchini kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zinazoongoza sekta hiyo ili kuongeza ufanisi katika kuongeza pato linalotokana na madini hayo. Kauli hiyo ameitoa wakati akifungua mafunzo kwa viongozi na maafisa waandamizi wa tume hiyo, mafunzo yanayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA.
|