Diamond Platinumz alishangazwa na wazalishaji wake wa muziki wiki iliopita walipoingia katika nyumba yake na keki iliokuwa na nembo ya kuadhimisha hatua muhimu ya nyota huyo wa Tanzania.
Huku akipigwa picha akivalia nguo , mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 30 aliambiwa na kundi lake kwamba ndiye msanii wa kwanza katika jangwa la sahara kupata views bilioni moja katika chaneli ya Youtube.
Katika kipindi cha miaka 10 iliopita, mwanamuziki huyo alieshinda mataji kadhaa amekuza muziki wa bongo fleva kuwa maarufu – muziki wa kipekee wa Tanzania unaotoa nyimbo za kimapenzi zilizochanganywa na midundo ya kisasa inayotokana na muziki wa jadi wa taarab kutoka pwani ya Afrika.
Diamond Platinumz ni mwanamuziki alie na bidii na maonyesho yake huvutia mashabiki wengi, kulingana na DJ Edu, ambaye amekuwa mtangazaji wa kipindi cha runinga cha kila wiki cha muziki wa Afrika cha BBC.
Huku akiwa na asilimia 43 ya mashabiki miongoni mwa raia milioni 55 nchini Tanzania wanaoweza kuingia katika mtandao, kupitia simu aina ya smartphones, kuna mashabiki wengi wanaopenda muziki wa bongo fleva walio tayari kusikiliza muziki wake wa mapenzi.
Wanamuziki wengine kama Harmonize pia nao wamebobea katika YouTube.
Je Views bilioni moja ni nyingi kiasi gani katika YouTube?
Ni vigumu kubaini umuhimu hasa wa nambari bilioni moja , ikizingatiwa kwamba Diamond Platinumz ana wafuasi wengi katika mtandao wa Instagram ikilinganishwa na wafuasi wake katika YouTube ambao ni milioni 9.7 ikilinganishwa na milioni 3.7.
DJ Edu anasema kwamba Instagram ni mtandao wenye ushawishi mkubwa kuhusu mtindo wa maisha na majukwaa mengine kama vile TikTok , ambayo inaruhusu sekunde 30 za hakimiliki ya utumizi wa bure wa nyimbo – ni njia nzuri ya kuwanasa wafuasi vijana.
”Nyimbo nyengine zinasambaa sana kupitia TikTok , kama wimbo mpya wa Diamond Platinumz kwa jina Quarantine”, anasema