NA.AYOUB MWIGUNE
Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania anayekipiga Klabu ya Aston Villa Mbwana Samatta amesema kuwa kutua kwake ndani ya Aston Villa kutaungwa mkono na watanzania wengi watakaoishabikia timu hiyo.
Samatta amesaini mkataba miaka minne na nusu ndani ya Aston Villa akitokea Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji.
Aston Villa leo itakuwa na kibarua kigumu mbele ya Leicester City wakiwa nyumbani ikiwa ni mchezo wa FA, Dean Smith, Kocha Mkuu wa Villa amesema kuwa Samatta anaweza kuanza leo.
Aston Villa wanatakiwa kushinda mechi ya Leo ili kusonga mbele baada ya mchezo wa Kwanza kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1.