Japan imepokea mwenge wa Olimpiki kutoka kwa Ugiriki katika makabidhiano ambayo hayakuwa na shamrashmra, kutokana na hofu ya mripuko wa virusi vya corona.
Muogeleaji wa zamani wa Japan Naoko Imoto anayeishi Ugiriki alipokea mwenge huo wiki iliyopita katika uwanja uliokuwa mtupu, ambao ulitumika katika mashindano ya kwanza ya michezo ya sasa ya Olimpiki mwaka 1896.
Mkuu wa kamati ya Olimpiki ya Ugiriki Spyros Capralos alisema wanatumai mwenge huo utaweza kukizima kirusi cha corona wakati mwenzake wa Japan Yoshiro Mori akizungumza kwa njia ya vidio.
Kamati ya kimataifa ya Olimpiki inaendelea na maandalizi ya michezo hiyo iliyopangwa kufanyika kuanzia Julai 24 hadi agosti 9, licha ya kitisho cha dunia cha COVID-19.
Mwenge huo wa Olimpiki unatarajiwa kuwasili Japan kesho Ijumaa.