Kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro Willbroad Mutafungwa akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani (Picha na Vedasto George)
Na Vedasto George, Morogoro
Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro limekamata komputa 21 kati ya 23 zilizokuwa zimeibwa shule ya msingi Msamvu B ambazo zililetwa shuleni hapo kwa ajili ya kufundishia wanafunzi
Akizungumza na Wanahabari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Willbroad Mutafungwa amesema watuhumiwa watatu tayari wamekamatwa na kufanyiwa mahojiano ambapo wamekiri kuhusika katika tukio hilo huku mlizi wa shule hiyo akiwa ametokomea kusikojulikana
“Lakini katika hali ya kushangaza tukapata taarifa kuwa mlinzi aliyekuwa amekabidhiwa dhamana ya kuwa mlinzi katika shule hiyo na mali zingine za shule hiyo ametoweka na wezi badala ya kulinda” amesema Mutafungwa
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Msamvu Bw. Elidad Methew amelishukuru Jeshi la polisi kwa kufanya kazi yake kwa weledi mkubwa na kuelezea namna komputa hizo zilivyokuwa zinatumiwa, huku baadhi ya wanafunzi wakieleza furaha yao mara baada ya kukamatwa kwa komputa hizo
Katika tukio jingine Kamanda Mutafungwa amesema kwa kushirikiana na askari wa wanyamapori wamemkamata mtu mmoja akiwa na pembe moja ya ndovu yenye uzito wa kilogramu 3 ambayo ilikuwa ikisafirishwa kwa kutumia pikipiki yenye namba za usajiri MC 818 BTU.