Bill na Melinda Gates wametangaza
talaka yao baada ya miaka 27 ya ndoa, wakisema “hatuamini tena tunaweza
kuwa pamoja kama wanandoa”.
“Baada ya kufikiria sana na kufanya kazi nyingi juu ya
uhusiano wetu, tumefanya uamuzi wa kumaliza ndoa yetu,” wawili hao walisema
katika ujumbe wa twitter .
Walikutana kwa mara ya kwanza miaka ya 1980 wakati Melinda
alipojiunga na kampuni ya Bill ya Microsoft.
Wanandoa hao mabilionea wana watoto watatu na kwa pamoja
wanaendesha Wakfu wa Bill & Melinda Gates.
Shirika hilo limetumia mabilioni kufadhili kampeni mbalimbali
ikiwemo magonjwa ya kuambukizana na kuhamasisha chanjo kwa watoto.
Wawili hao – pamoja na mwekezaji Warren Buffett – wanahusika na
mpango wa Ahadi ya Kutoa, ambao unawataka mabilionea kujitolea kutoa utajiri wao
mwingi kwa malengo ya kuwafaidi watu .