Hatua hiyo imejiri baada ya kuchapishwa kwa matokeo ya
uchunguzi wa miaka miwili kuhusu mtindo wenye utata wa baadhi ya watu
kuendeleza uzalishaji wa simba ambao wamezuia katika mbuga za binafsi na
majumbani .
Iligundulika kwamba mtindo huo ulihatarisha juhudi za uhifadhi
wa wanyama hao na pia madhara kwa wafugaji .
Serikali ya Afrika Kusini imekubali mapendekezo ya jopo
lililofanya uchunguzi huo hatua ambayo huenda haitawafurahisha wadau katika
sekta ya uwindaji.
” Ripoti hiyo inapendekeza kupigwa marufuku kwa mipango
ya kuzalisha simba au kuwaweka majumbani ‘ waziri wa Mazingira Barbara Creecy
amesema .
” Hatutaki kuzalishwa kwa simba waliozuiliwa majumbani
,kuwekwa kwao kama wanyama wa nyumbani au matumizi ya wanyama hao kama vivutio
vya utalii wakiwa wamzuiliwa .
Hata hivyo amesema kuwindwa kwa simba wa porini kutaruhusiwa
kuendelea . Shughuli hiyo huleta pato kubwa la utalii kwani maelfu ya watu
husafiri kwenda Afrika Kusini kuwawinda simba wa porini .
Jopo hilo lilipewa jukumu la kutathmini sera za Afrika kusini
kusimamia uwindaji wa simba ,chui , ndovu na vifaru.
Kuhusu pembe za vifaru na ndovu, jopo hilo lilipendekeza
mazungumzo na nchi nyingine za kusini mwa Afrika kabla ya kuamua ikiwa zinaweza
kutolewa.
Takriban simba 8000 wanaaminika kuwa majumbani nchini Afrika
Kusini ikilinganishwa na simba 3500 walio msituni .
Wanaounga mkono kuwekwa kwa simba majumbani wanasema ni hatua
inayoweza kuwatunza wanyama hao lakini wakosoaji wanadai ni matesi dhidi ya
wanyama hao wanaofaa kuwa porini Shirika la kutetea maslahi ya wanyama World Animal Protection limetaja uamuzi huo wa Afrika kusini kama ‘ushindi katika kuwalinda wanyama wa
pori’