Binadamu wa kwanza kufanyiwa jaribio ya chanjo ya kinga dhidi ya virusi vya corona ameanza kufanyiwa jaribio hilo nchini Marekani.
Wagonjwa wanne walidungwa sindano ya virusi katika kituo cha utafiti Kaiser Permanente mjini Seattle, Washington, limeripoti shirika la habari la Associated Press.
Chanjo hiyo haiwezi kusababisha Covid-19 lakini ina jeni la virusi ambavyo vinaweza kusababisha ugonjwa.
Wataalamu wanasema itachukua miezi mingi kujua ikiwa chanjo hii, au utafiti mwingine, utafanikiwa.
Mtu wa kwanza kujitolea kupata dozi ya kwanza ya utafiti huo siku ya Jumatatu ni mama wa watoto wawili mwenye umri wa miaka 43 mkazi wa Seattle Washington.
“Hii ni fursa ya kufurahisha kwangu mimi kuweza kufanya kitu fulani,” alisema mama huyo aliyetambuliwa kama Jennifer Haller katika mazungumzo na shirika la habari la AP.
Wanasayansi kote duniani wanaharakisha utafiti wao kujaribu kupata chanjo au tiba ya coronavirus.
Na jaribio hili la kwanza kwa binadamu,lililodhaminiwa na Taasisi ya Kitaifa ya Afya nchini Marekani, umefanyika kando ili kuangalia kile ambacho kwa kawaida kingekua kikifanyika kuhakikisha chanjo inaweza kusababisha kuchochewa kwa kinga ya mwili katika wanyama.
Lakini kampuni ya teknolojia ya masuala ya vimelea wa magonjwa ambayo ndiyo inayoendesha utafiti huo, Moderna Therapeutics, inasema kuwa chanjo imekwishakutengenezwa kwa kutumia mchakato uliojaribiwa na kupimwa.
Binadamu wa kwanza kufanyiwa jaribio ya chanjo ya kinga dhidi ya ugonjwa wa corona ameanza kufanyiwa jaribio hilo nchini Marekani
Wagonjwa wanne walidungwa sindano ya virusi katika kituo cha utafiti Kaiser Permanente mjini Seattle, Washington, limeripoti shirika la habari la Associated Press.
Chanjo hiyo haiwezi kusababisha Covid-19 lakini ina jeni la virusi ambavyo vinaweza kusababisha ugonjwa.
Wataalamu wanasema itachukua miezi mingi kujua ikiwa chanjo hii , au utafiti mwingine, utafanya.
Mtu wa kwanza kujitolea kupata dozi ya kwanza ya utafiti huo siku ya Jumatatu ni mama wa watoto wawili mwenye umri wa miaka 43 mkazi wa Seattle Washington.
“Hii ni fursa ya kufurahisha kwangu mimi kuweza kufanya kitu fulani ,” alisema mama huyo aliyetambuliwa kama Jennifer Haller katika mazungumzo na shirika la habari la AP.
Wanasayansi kote duniani wanaharakisha utafiti wao kujaribu kupata chanjo au tiba ya coronavirus.
Na jaribio hili la kwanza kwa binadamu, lililodhaminiwa na Taasisi ya Kitaifa ya Afya nchini Marekani , umefanyika kando ili kuangalia kile ambacho kwa kawaida kingekua kikifanyika kuhakikisha chanjo inaweza kusababisha kuchochewa kwa kinga ya mwili katika wanyama.
Lakini kampuni ya teknolojia ya masuala ya vimelea wa magonjwa ambayo ndiyo inayoendesha utafiti huo -Moderna Therapeutics, inasema kuwa chanjo imekwishakutengenezwa kwa kutumia mchakato uliojaribiwa na kupimwa.
Dkt John Tregoning, mtaalamu katika magonjwa ynayoambukia katika taasisi ya Imperial College mjini London, Uingereza,amesema: “Chanjo hii imetumia Teknolojia iliyokuwepo awali.
“Imefanyika kwa kiwango cha hali ya juu, kwa kutumia vitu ambavyo tunavyofahamu ni salama kuvitumia katika watu na wale wanaoshiriki katika jaribio hili watakua wakifuatiliwa kwa karibu sana.
“Ndio, hili limefanyika haraka sana-lakini ni mbio dhididi ya virusi, sio dhidi ya kati ya mwanasayansi na mwanasayansi , na inafanyika kwa manufaa ya binadamu .”
Chanjo halisi ya virusi kama vile vinavyosababisha magonjwa kama surua(ukambi) hutengenezwa kutokana na virusi vilivyodhoofishwa au vilivyokufa.
Lakini chanjo ya mRNA-1273 haijatengenezwa kutokana na virusi vinavyosababisha Covid-19.
Badala yake, inajumuisha kipande kifupi cha aina ya jeni iliyonakiliwa kutoka kwa virusi ambavyo wanasayansi wamemeweza kuvitengeneza katika maabara.
Unaweza pia kusoma:
- Nini kinafanyika Coronavirus inapoingia mwilini?
- Je juhudi za kutafuta chanjo ya coronavirus zimefika wapi?
- Tanzania yathibitisha kuwa na kisa cha kwanza cha corona
Chanjo hii huenda ikasaidia mwili kujitengenezea mfumo wake wa kinga wa kupigana na ugonjwa halisi.
Waliojitolea kufanyiwa jaribio la chanjo walipewa dozi tofauti za jaribio la chanjo.
Kila mmoja atadungwa sindano mbili za virusi kwa ujumla, baada ya siku 28, kwenye mshipa wa sehemu ya juu ya mkono.
Lakini hata kama vipimo vya awali salama vimefanikiwa, bado inaweza kuchukua hadi miezi 18 kuweza kuwa na uwezekano wowote wa chanjo kuweza kupatikana kwa umma.