Na: Josephine Malango
Imeelezwa kuwa teknolojia ya kulima eneo dogo kwa uzalishaji mkubwa wa tija inaweza kuwa moja wapo ya njia ya kutatua migogoro ya ardhi katika maeneo yenye migogoro ukiwemo mgogoro ya ardhi mkoani wa morogoro uliodumu na kwa muda mrefu.
Hayo yamesemwa na katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Kalobelo wabaada ya kutembelea mashamba darasa ya mradi wa uhakiki na usambazaji wa jitihada shirikishi za kuleta mapinduzi ya kilimo vijijini [RIPAT], kutoka kwa watalaamu wa chuo kikuu cha sokoine cha kilimo sua wakati wa wamaonesho ya kilimo katika kijiji cha mlali wilaya ya Mvomero mkoa wa Morogoro .
Amesema kuwa teknolojia aliyoiona katika mashamba darasa hayo ya RIPAT sua yana tija kubwa kwa matumizi ya ardhi ndogo kwa uzalishaji wa tija na anaamini kupitia teknolojia hiyo rahisi ikitumiwa vizuri katika eneo la kilimo lililopo mkoani Morogoro itasaidia uzalishaji wa tija na ziada ya kulisha nchi kwa kuwa Mkoa wa Morogoro ni moja ya Mkoa unaochangia katika ghala la taifa la chakula.
Ameongeza kuwa uwepo wa Chuo kikuu Sua Morogoro ni fursa hivyo wakulima waitumie kwa kuwa mkoa huo una fursa adhimu ya mashamba ya wakulima kutembelewa na maprofesana wakulima hao wahakikishe teknolojia hizo wanaziishi kwa vitendo ili lengo la mradi huo wa RIPAT kwa kushirikiana na RECODA la kuongeza mwitikio wa teknolojia kwa wakulima na wafugaji uwe na uhakika wa chakula na kipato kutimia.
Amewasisitiza wakulima wote wa Mkoa wa Morogoro hatawale ambao hawapo sehemu ya mradi kuona umuhimu wa kuwatumia wataalam wa sua ili kauli mbiu ya NJAA NA UMASIKINI KUWA HISTORIA INAWEZEKANA, iendane na vitendo kwa kulima maeneo madogo na kutoa mavuno yenye tija badala ya mazoea yaliyokuwepo ya kusema mameno matupu ya mkoa wa morogoro unazalisha huku kukiwa hakuna uhalisia.
Kwa upande wake makamu wa mkuu wa Chuo kikuu cha Sokoine cha kilimo Sua Prof. Raphael chibunda amesema amefurahishwa kuona kwa vitendo na uhalisia namna mradi wa RIPAT ulivyo na mafanikio kwa wakulima katika maeneo hayo na kuwapongeza watafiti wa mradi wa RIPAT kwa kutekeleza utafiti huo kwa vitendo na siyo maigizo.
zaidi bofya hapa