Na.Vedasto Geoge
Balozi wa China nchini Tanzania PWANG KE amesema kuwa nchi yake itaendelea
kushirikiana na Tanzania katika kuimarisha na kukuza sekta mbalimabali ikiwemo
Kilimo ili wakulima waweze kunufaika na mazao yao na Taifa kiujumla.
PWANG KE amesema hayo wakati akifunga mafunzo ya wakulima kwa kilimo cha
mpunga Dakawa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro yaliyokuwa
yakiendeshwa na Kituo cha Kukuza Teknolojia za Kilimo cha China ambapo amesema
Sekta ya Kilimo ni muhimu sana katika uchumi wa taifa na kuwataka wakulima kuendelea
kujikita katika kilimo biashara.
Aidha PWANG KE amesema kuwa china ipo tayali kununua korosho zinazo zalishawa
nchini Tanzania, na kuongeza kuwa katika maonyesho ya kibiashara ya nayoendelea
nchini China nchi ya Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi washiliki na kupata nafasi
ya kutembelewa na Raisi wa nchi hiyo.
Kwaupande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa kilimo Tanzania (TARI)
Dakawa Bw. Andrew Ngereza na Mkurugenzi wa Wakala wa Usambazaji mbegu za
kilimo nchini (ASA) Bi. Sofia Kashenge wamesema China imekuwa nchi inayo toa
msaada mkubwa katika kuakikisha kilimo nchini kinakuwa na tija kwa mkulima na taifa,
huku wakimwakikisha Balozi wa China kuendelea kushilikiana ili sekta ya kilimo iweze
kukua Zaidi.
Baadhi ya wanufaika wa mafunzo ya kilimo cha mpunga akiwemo Nassibu Katoto
Mkulima kiongozi katika skimu ya Wami Dakawa na Laizer Sulle Afisa Kilimo Kijiji