Na: Farida Mkongwe
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Philip Mpango kesho Mei 27 atakuwa Mgeni Rasmi kwenye ufungaji wa Maonesho ya Wiki ya Hayati Edward Moringe Sokoine yanayofanyika kwenye Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA mjini Morogoro.
Kufuatia ugeni huo mapema Mei 25 mwaka huu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigella amewataka wakazi wa mkoa wa Morogoro na maeneo ya jirani kujitokeza kwa wingi kwenye viwanja vya SUA kumlaki na kumsikiliza kiongozi huyo.
Hii ni mara ya kwanza kwa Makamu wa Rais Mh. Dkt. Mpango kufika mkoani Morogoro tangu kuanza kuutumikia wadhifa huo.
Maonesho ya Wiki ya Kumbukizi ya Hayati Edward Moringe yalifunguliwa rasmi na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Mashimba Ndaki Mei 24 na yatafungwa rasmi na Makamu wa Rais Mh. Dkt. Philip Mpango siku ya Alhamis Mei 27 mwaka huu.