Na.Vedasto George.
Utendaji kazi uliotukuka pamoja na Tafiti mbalimbali zinazofanywa
na Chuo cha Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA vimekiwezesha chuo hicho kuweza
kupanda hadhi ya ubora kwa Vyuo Vikuu barani Afrika kutoka nafasi ya sitini na
saba kwa mwaka jana hadi kufikia nafasi ya 53 kwa mwaka huu wa 2021.
Hayo yamebainishwa hivi karibuni na Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha
Sokoine cha Kilimo SUA Prof.Raphael Chibunda wakati akitoa salamu na kuzungumza
na wanachama wa chama cha wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya
juu,Sayansi,Teknolojia na Utafiti RAAWU Tawi la SUA katika Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi duniani
ambayo ufanyika kila ifikapo tarehe moja ya mwezi wa tano kila mwaka.
“Chuo chetu kimeweza kupanda hadhi katika vyuo vikuu vya afrika
tulikuwa chuo cha sitini na saba mwaka jana lakini januari ya mwaka huu wa 2021
tumekuwa wa 53 ambapo kwetu tumeona ni mabadiliko makubwa lakini lengo letu
ndani ya miaka miwili inayo kuja ni kuweza kuingia kwenye listi ya vyo vikuu
ishirini bora.”Alisema Prof.Raphael Chibunda
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za
Elimu ya Juu,Sayansi,Teknolojia na Utafiti RAAWU Tawi la SUA Bi.Gaudensia
Donati amebainisha kuwa maadhimisho hayo ya siku ya wafanyakazi Duniani
uadhimishwa ili kukukbuka harakati za
kudai haki kwa wafanyakazi zilizopelekea kuundwa kwa Vyama vya wafanyakazi ambavyo
msingi wake mkubwa ni kuweka mazingira mazuri maala pakazi na kuweza
kujadiliana na mwajiri ili wafanyakazi waweze kilipwa ujila wao sahihi.
“Hapo zamani wafanyakazi walikuwa wanafanya kazi nzito wanatumikishwa lakini walikuwa wanapewa ujira mdogo usio kidhi mahitaji yao na kwa nchi yetu kamanda ambaye tunamkumbuka aliweza kupambana na kudai haki za wafanyakazi na vuguvugu la vyama vya wafanya kazi ni hayati Mfaume Kawawa yeye ndiye alifanya vuguvugu kubwa na alihangaika sana kuona Tanzania kunakuwa na msingi wa vyama vya wafanyakazi ili nao waweze kuongea na mwajiri” Alisema Bi.Gaudensia Donati.
Naye Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu,Sayansi,Teknolojia na Utafiti RAAWU Tawi la SUA Bi.Catherine Ogessa amekiomba Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kuendelea kudumisha utawala bora katika kutatua kero za wafanyakazi ikiwemo kuboresha mazingira ya kazi kwa maana ya vitendea kazi na usalama kazini.
Katika kutambua mchango na kazi kubwa inayofanywa na wafanyakazi katika
Chuo hicho cha SUA kimetoa tunzo kwa wafanyakazi bora 56 kati yao sita ni
wafanyakazi hodari.
Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi kwa Mkoa wa Morogoro yamefanyika
Manispaa ya Morogoro yakibebwa na kauli mbiu isemayo MASILAHI BORA, MISHAHARA JUU KAZI IENDELEE, wito ukitolewa kwa serikali kuangalia namna bora kuboresha mishahara na madaraja ya wafanyakazi na kudhibiti ukandamizaji kwa wafanyakazi kwa baadhi ya taasisi.