SUA YA KWANZA KUPATA RUZUKU KUBWA BARANI AFRIKA
Na:TATYANA CELESTINE Imeelezwa kuwa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) ni cha kwanza barani afrika kupata ruzuku kubwa kutoka shirika la kutoa misaada la watu wa marekani (usaid) misaada inayosaidia kuimarisha miundombinu na taaluma katika chuo hicho……………………….
Bofya kichwa cha habari kwa habari zaidi……. |
NA: TATYANA CELESTINE
Imeelezwa kuwa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) ni cha kwanza Barani Afrika kupata ruzuku kubwa kutoka Shirika la kutoa misaada la watu wa Marekani (USAID) misaada inayosaidia kuimarisha miundombinu na taaluma katika chuo hicho.
hayo yamesemwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Prof. Gerard Monela wakati wa mazungumzo na Balozi wa Afrika ya Kusini nchini Tanzania Mhe. Thamsanqa Mseleku alipotembelea chuoni sua mapema wiki iliyopita
Prof: Monela amesema kuwa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa mujibu wa hati idhini yake kimepewa ruhusa ya kufanya tafiti na kushirikiana na wengine wanaojihusisha na masuala ya kilimo, ufugaji na uvuvi ili kuhakikisha kila tafiti inapofanyika iweze kutoa mchango kwa jamii ili kutatua changamoto mbalimbali zinzoikabili jamii.
aidha Prof. Monela amemsifu waziri mkuu wa tanzania mhe: Mizengo Peter Pinda kwa kuunga mkono chuo katika suala zima la ufugaji na maendeleo ya mazao ya asali na pia kusaidia kuitafutia masoko ndani na nje ya nchi kwani ni njia mojawapo itakayopelekea kukuza soko na ufugaji wa asali nchini tanzania
amesema kuwa serikali inajitahidi kutatua changamoto mbalimbali zinazokikabili chuo pamoja na ukongwe wake hivyo ameomba mashirika kujitokeza kukisaidia chuo kikuu cha sokoine cha kilimo sua ili kuondoa changamoto za vifaa na kufanya chuo kiweze kutoa taaluma iliyo bora kila wakati.
kwa upande wake Balozi wa Afrika ya Kusini nchini mheshimiwa Thamsanqa Mseleku amesisitiza ni vema kutengeneza mahusiano mazuri na wadau wengine kwa kuwatembelea na kuona wanavyofanya kazi zao hasa zinazohusu jamii
aidha amesema kuwa amekuwa akifuatilia kwa ukaribu Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kutuma wawakilishi mbalimbali toka afrika ya kusini kuja nchini kufanya kazi na SUA na imekuwa ni faida kubwa na imepelekea kuwa na ari ya kutaka kufahamu historia ya sua na kudumisha ushirikiano kati ya Chuo na nchi ya Afrika ya Kusini