Na: Josephine Mallango
Wiki ya kuhamasisha matumizi sahihi ya dawa za antibiotic yazinduliwa rasmi nchini katika kuelekea maadhimisho ya kidunia wiki hiyo itaanza Novemba 18-24,mwaka huu ambapo athari zaidi za matumizi holela ya dawa za antibiotic zimeendelea kuzikumba nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.
Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Ellias Kwesi akizungumza wakati wa kutoa tamko la kuhamasihsa matumizi sahihi ya dawa za Atibiotiki nchini kuelekea maadhimisho ya kidunia
Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Eliasi Kwesi amezindua rasmi shughuli za kuhamasisha matumizi sahihi ya dawa za Antibiotiki katika kuelekia wiki hiyo duniani kote kwa kusoma tamko rasmi kwa niaba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu ambapo ameiasa jamii kuelewa athar i na tatizo kubwa ambalo limekuwa likiongezeka kila kukicha duniani kote.
Amesema matumizi sahihi ya dawa za antibiotic yamepelekea kuzuilika kwa vifo vingi vinavyosababishwa na magonjwa ya kuambukiza kutokana na uwezo mkubwa wa dawa hizo toka kuanza kutumika mwaka 1940 ambapo tafiti zimeonyesha dawa ya penicilini iliweza kutibu nimonia na maambukizi ya vidonda kupona kwa asilimia 90 % toka asilimia 10 iliyokuwepo kabla ya kuanza kwa matumizi ya antibiotic .
Dkt. Kwesi ameongeza kuwa uwepo wa sasa wa matumizi mabaya ya dawa hizo kwa binadamu na wanyama umepelekea vimelea vya magonjwa ya kuambukiza aina ya bakteria vimejenga usugu ambapo report ya benki ya dunia ya mwaka 2017 imebainisha kuwa zaidi ya watu laki 700,000 wanafariki kila mwaka kutokana na usugu wa dawa hizo na hatua madhubutu zisipochukuliwa haraka watu milioni 10 watafariki kila mwaka kutokana na usugu wadawa hizo ifikapo mwaka 2050.
“Hali ya usugu wa vimelea dhidi ya dawa aina ya antibiotic inaweka mashaka makubwa ya kupoteza nguvu kazi ya Taifa hili kwa kusababisha vifo kutokana na kuongezeka kwa magonjwa sugu yasiyotibika kwa kutumia dawa zilizokuwa na uwezo wa kutibu, kuongezeka kwa umasikini kutokana na kuugua muda mrefu na kutumia dawa ghari zaidi na pia kuongezeka kwa vifo vya mifugo na uzalishaji hafifu wa chakula na pia kugharimu Taifa fedha nyingi ambazo zingeweza kutumika kuleta maendeleo ” amesema Dkt. Kwesi.
Kaimu mganga mkuu huyo ameongeza kuwa Lengo la wiki hii litakuwa ni kusisitiza kuongeza uelewa juu ya matumizi sahihi ya dawa za antibiotic kwa kupunguza matumizi yasiyostahili na kuzuia ongezeko la usugu wa vimelea dhidi ya dawa hizi ili kujiweka katika mazingira salama huku akiitaka jamii kuzingatia matumizi sahihi kwa kutumia dawa kwa mujibu wa wataalamu na siyo kiholela na kwa upande wa watoa dawa kote nchini kuandika dawa kwa kufuata mwongozo wa matibabu wa mwaka 2017 wa kutumia majina halisi ya dawa .
Kwa upande wa serikali ameseam imendaa mipango na miongozo mbalimbali ili kutekeleza kazi kwa usahihi ikiwemo mpango wa Taifa wa kupambana na usugu wa dawa dhidi ya vimelea mbalimbali Antimicrobial ( 2017-2022) pamoja na kuagiza vituo vyote vya huduma ya afya kutekeleza miongozo ya kukinga na kuzuia maambukizi ambayo ni muhimu sana kuzuia usugu katika sehemu zao za kazi .
Dkt. Kwesi alizitaka Wizara zingine wadau wakiwemo Mawaziri wa Mifugo na uvuvi,, Kilimo na Mazingira kwa pamoja kufanya kampeni zinazolenga kuongeza uelewa wa jamii juu ya matumizi sahihi na athari zitokanazo na matumizi holela ya dawa kwa binadamu na mifugo kwa kuwa matumizi sahihi ya antibiotic kwa sasa ni faida ya kizazi kijacho kwa matumizi endelevu ikiwa kila mmoja atatimiza wajibu wake .
Ujumbe wa mwaka huu kuelekea maadhimisho ya wiki ya matumizi sahihiya antibiotic ni “uwepo wa dawa za Antibiotic kwa siku zijzazo unatutegemea sote “ ambapo wakati wa tam,ko hilo la serikli wadau mbalimbali wakiwepo wakiwemo wawakilishi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Shirika la Afya(WHO), Shirika la Chakula (FAO) na Shirika la Wanyama (OIE) walieleza wanashirikiana kwa pamoja na Serikali ya Tanzania katika kutatua changamoto hiyo.
Wadau mbalimbali kutoka mashirika ya kimataifa ikiwemo WHO,FAO na Shirika la wanyama (OIE) wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi aliyevaa suti ya blue Dkt. Eliass Kwesi.