Na: Tatyana Celestine
Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphel Chibunda amewataka Wastaafu na wanataaluma wa SUA kuhakikisha wanazingatia maadili ya ufundishaji ili kuongeza ubora wa elimu inayotolewa chuoni hapo.
Prof. Chibunda amesema kuwa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kina heshima na thamani kubwa katika Kanda ya Mashariki kwasababu ya ubora wa elimu kinayotoa hivyo Wastaafu wanatakiwa kuwa chanzo cha maarifa kwa waajiriwa wapya chuoni hapo.
Amesema hayo wakati wa sherehe iliyoandaliwa na shule Kuu ya Uchumi Kilimo na Stadi za Biashara yenye lengo la kuwakaribisha waajiriwa wapya, mwaka mpya, pamoja na kuwaaga Wastaafu ambao wametumikia chuo hicho ambapo Wafanyakazi wa SUA pamoja na idara zingine katika chuo hicho wamehudhuria.
Aidha Prof. Chibunda amewataka walimu wapya wazingatie maadili ya kuwa walimu wa Chuo Kikuu kwa kutenda haki na kufundisha kwa bidii kwa kuwa matarajio ya chuo ni kufanya shule kuu hiyo ibadilike iwe Ndaki kutoka na jitihada zilizofanywa na kufanikisha program moja ambayo imekwishapitiwa na TCU na inatakiwa kuanza mwaka 2020.
“Mwalimu wa Chuo Kikuu ni Jaji unatunga mtihani unausahihisha wewe na unasema huyu kafeli ama huyu kapasi na consequence yake ni kubwa unaposema huyu kafeli inamaana kuwa umefikisha matarajio yake mwisho kielimu,kwa hiyo ukifanya katika mazingira ambayo umeonea, hujatenda haki huyu mtu utakuwa umemfanyia dhuluma kubwa sana” amesema Prof. Chibunda.
Ameendelea kusisitiza kuwa …………… “Na nishukuru Amidi, nilipokuja kufanya mkutano na walimu wa school hii tumejadili na tumekubaliana kuanzisha program mpya, program moja tuliyokubaliana ya Agriculture Investment and Banking imepitiwa na TCU mwaka huu inakwenda kuanza” amesema Prof. Chibunda.
Nae Amidi wa Shule Kuu ya Uchumi Kilimo Prof. Adam Akyoo amemshukuru Mkuu wa chuo hicho kwa jitihada na kutimiza ahadi yake hata kabla muda wake kwisha kwani amewezesha kumalizia jengo la PHD pia kuhakikisha makubaliano ya kuanza kwa program yanafikiwa kwa wakati.
Vilevile amewataka wafanyakazi walioko chini yake kuheshimu jitihada za mkuu wao kwa kufanya kazi kwa bidii na kuona nafasi hiyo kama ni ya kipekee.
FUATILIA KATIKA PICHA NA MATUKIO