Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH imetoa tuzo za ushindi wa pili kwa Waandishi wa Habari za Sayansi nchini Tanzania kutoka kituo cha utangazaji cha SUAMEDIA kilichopo mkoani Morogoro.
Tuzo hizo zinetolewa jana novemba 13, 2019 Jijini Dar es salam na Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt. Amos Nungu na kuhudhuriwa na waandishi mbalimbali wa habari nchini na wadau wa Sayansi kutoka Taasisi na mashirika mbalimbali ya ndani na nje ya nchi
Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt. Amos Nungu amewataja washindi hao kuwa ni Josephine Mallango na Farida Mkongwe kutoka suamedia ambapo Farida Mkongwe amekuwa Mshindi wa Pili kwa Muandaaji bora wa Vipindi vya Sayansi kwa Upande wa Televisheni kwa mwaka 2019 wakati Mshindi wa Kwanza ni Sifuni Mshana wa ITV.
Nae Josephine Mallango ameibuka Mshindi wa Pili kwa Upande wa Redio kama Muandaaji bora wa Vipindi vya Sayansi kwa mwaka 2019 wakati Mshindi wa Kwanza ni Devi’s Rwenyagila kutoka East African Redio.
Tuzo hizo zimeanza kutolewa 2017 kwa lengo la kuhamasisha waandishi wa habari za kisayansi kuhabarisha umma juu ya matokeo ya utafiti wa kisayansi ambapo mwaka jana mshindi wa OFAB alikuwa mwandishi Calvin Gwabara kutoka SUAMEDIA CHUO KIKUU CHA SOKOINE MOROGORO.
Kwa taarifa zaidi bofya hapa
https://www.costech.or.tz