Na Vedasto George.
Chama cha Afya ya Jamii nchini TPHA kwa kushirikiana na Serikali kimesema kitaendelea kutoa tafiti mbalimbali zinazo husu Afya ili kuwawezesha wananchi kutambua na kuelewa Afya zao ikiwa ni pamoja na kutambua magonjwa yatokanayo na wanyama kwenda kwa binadamu.
Mwenyekiti wa wa chama TPHA Dr. Bashombo Mkamba
Akizungumza katika mkutano wa 36 wa mwaka uliowakutanisha wanachama 45 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania, Mwenyekiti wa wa chama hicho Dr. Bashombo Mkamba amesema lengo la kuanzishwa kwa chama hicho ni kuhamasisha watanzania juu ya matumizi ya taarifa zilizofanyiwa utafiti juu ya Afya ya binadamu.
Tunaleta tafiti zinazowasilishwa katika mada mbalimbali kama ulivyoona leo ambapo tafiti nyingi zinatoa majibu au matokeo yanatusaidia kuona kwa namna gani tunaweza tukazitumia huko tunakokwenda na kama mnavyojua kwasasa tunaenda kwenye Tanzania ya Uchumi na Viwanda hivyo ni vema tukalinda Afya zetu ili kutufanya tuwe na nguvu lakini kingine ili watu wajikinge na kupata matibabu lazima wapate habari. alisema Dr. Bashombo Mkamba
Akiwasilisha mada ya usugu wa madawa katika mkutano huo Prof. Japheti Killewo kutoka Chuo Kikuu cha Muhimbili na mwanzilishi wa TPHA amesema kuna magonjwa ambayo huanzia kwa wanyama na kuwasumbua binadamu na hivyo kuomba kuwepo kwa mpango shirikishi ili kuweza kuyadhibiti yasiweze kuleta madhara zaidi.
Kwaupande wake Mratibu wa mradi wa kuzuia Madhara ya pombe kutoka chama Chama cha Afya ya Jamii Tanzania Bi . NJerina Jasitne amesema kuna matokeo chanya yatokanazo na tafiti zinazo fanywa na chama hicho tangu kuanzishwa.
Matokeo yake ni makubwa tunayaona kwa sababu chama kimeanza tangu mwaka 1980 na ili ni kongamano la 36 ni ujumbe mwingi sana tumetoa kwa jamii kutokana na Afya ambayo inausiana na mambo mbalimbali si magonjwa peke yake, Afya inajumuisha mazingira pia, tunafikisha ujumbe kwa jamii kwa njia ya makongamano haya yanayojumuisha sekta mbalimbali za Afya,Elimu nk kwa sababu sisi atuchagui wanachama .alisema Jerina Jusitne Mratibu wa mradi wa kuzuia Madhara ya pombe kutoka chama Chama cha Afya ya Jamii Tanzania TPHA.
Prof. Japheti Killewo kutoka Chuo Kikuu cha Muhimbili na mwanzilishi wa TPHABaadhi ya Washiriki katika Mkutano wa 36 wa mwaka uliowakutanisha wanachama 45 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania
Baadhi ya Washiriki katika Mkutano wa 36 wa mwaka uliowakutanisha wanachama 45 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania
FUATILIA ZAIDI KATIKA VIDEO