Na: Tatyana Celestine
Imeelezwa tabia za kijografia kama ukame na oevu ni miongoni mwa sababu kubwa zinazosababisha Nzige kuzaliana kwa wingi na kuleta mazara mkubwa kwa jamii na hasa kwa wakulima
Hayo yamesemwa leo Marchi 4 na Mhadhiri Mwandamizi na Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Gratian Rwegasira ambaye pia ni mbobezi kwa wadudu hao warukao katika kipindi cha Mchakamchaka cha SUAFM na kufafanua kuwa baa la nzige linapotokea linawezekana kudhibitiwa ikiwa tu maandalizi yamefanyika kikamilifu na kwa wakati..
Sauti ya Prof Rwegasira
Prof. Rwegasira amesema kuwa tafiti zinaonesha kuwa nzige wapo wa aina mbili ambao ni wekundu na wale wa jangwani na wote huruka kwa makundi pia wana uwezo wa kuruka kwa umbali mrefu ikiwa ni pamoja na kutoka bara moja hadi jingine huku idadi ya yao inaweza kufikia hadi milioni 150
Prof Rwegasira amesema imekuwa vigumu kufuatilia utabiri unaotolewa mara kwa mara kuhusiana na kuonekana kwa nzige hao katika maeneo tofauti sababu ya upepo unaowachukua na wakati mwingine haujulikani unaweza kubadilika mwelekeo wao wakati gani.
Aidha ameendelea kusema kuwa mara nyingi nzige hao huruka na wakikutana na upepo hubebwa na endapo wakianguakia katika mazao ya kijani ambapo tafiti zinasema katika kilomita moja ya mraba nzige hao wanaouwezo wa kuteketeza chakula cha watu elfu 35 kwa siku
Hadi sasa baa la nzige halijafika nchini Tanzania tayari nchi za Ethiopia, Somalia, Kenya, Djibouti na Eritrea zimeathirika na wimbi la nzige limeenea maeneo ya kusini mashariki mwa Sudan Kusini na Uganda hadi kusini magharibi mwa Iran.
KATIKA VIDEO BOFYA HAPA CHINI