Ushirika wa wahitimu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUGECO) umetekeleza maadhimio ya Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kwa kutoa mafunzo kwa vijana takribani 80 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania pamoja kuanzisha benki za uzalishaji mbegu katika vijiji (Village seed banki) zitakazosaidia kupunguza uhaba wa mbegu bora kwa wakulima.
Akizungumza katika ghafla ya kuhitimisha mafunzo hayo ya siku tano, Afisa Mwandamizi kutoka Idara ya Sera na Mipango Wizara ya Kilimo REVELIAN NGAIZA amewataka vijana hao kwenda kuwafundisha vijana wenzao elimu hiyo kilimo cha kisasa na umwagilia, huku Mkurugenzi wa SUGECO Revocatus Kimario akieleza malengo ya kutoa elimu hizo kwa vijana hao.
Sauti ya REVELIAN NGAIZA… Afisa mwandamizi idara ya sera na mipango wizara ya kilimo
Sauti ya REVOCATUS KIMARIO… Mkurugenzi SUGECO
Aidha Mtaalam Mshauri wa SUGECO DKT Anna Temu amewataka vijana watumie ujuzi huo kwa kuanzisha vikundi vya kuzalisha mbegu bora kwa mikoa yote huku vijana waliohitimu wa mafunzo hayo kilimo cha umwagiliaji wa matone, usindikaji wa vyakula,kilimo mbogamboga na matunda Bi. TERESIA NGUBI na HOFFMAN MAHENGE wameelezea namna walivyopokea mafunzo hayo na jinsi watakavyoenda kuitumia elimu hiyo katika jamii zao.
Sauti ya DKT ANNA TEMU… mtaam mshauri sugeco
Sauti ya TERESIA NGUBI Mwanafunzi na HOFFMAN MAHENGE