Na: Calvin Gwabara
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kimeendeleza mkakati wake wa kuhakikisha wadau wa elimu inayoyotolewa chuoni hapo inawafikia watu wengi popote walipo kwa njia ya Masafa kwa kuzingatia ubora na gharama nafuu.
Mkakati huyo umebainishwa na Mratibu wa Kitengo cha Kusimamia ubora cha Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA, Dkt. Gratian Rwegasira wakati wa mafunzo ya siku tatu kwa Marasi wa Ndaki wapya,Wakurugenzi, Wakuu wa Idara, na viongozi wengine walioteuliwa hivi karibuni juu ya matumizi ya njia hiyo ya masafa ya utoaji wa Elimu chuoni hapo.
Mratibu huyo wa kitengo cha kuthibiti ubora SUA amefafanua kuwa watu wanaishi kwenye ulimwengu unaotegemea elimu na mahitaji ya elimu ni makubwa hivyo inatakiwa kutengeneza mifumo ambayo itawafikishia walengwa elimu bora kokote waliko kwa njia ya masafa.
‘’Elimu masafa ndio njia nzuri inayoweza kuwafikia watu wengi lakini elimu masafa lazima inde kwa kuzingatia ubora kwahiyo tunachokifanya ni kuwaelimisha viongozi waweze kujua mbinu za ubora na zinazohitajika na wapokwenda kutoa elimu masafa wawe wamezingatia hilo ambalo ndio kigezo muhimu katika kuhakikisha ubora wa elimu ya SUA haitikisiki na inaendelea kufuata misingi inayokubalika Kimataifa’’ Alisisitiza Dkt. Rwegasira.
Amesema mafunzo hayo yatasaidia waratibu wa kitengo hicho na Menejimenti ya Chuo kuweza kuhakikisha kile ambacho kimegharimiwa na kuazimiwa na Baraza la Chuo kinafanikiwa hasa katika matumizi ya utoaji wa elimu kwa masafa na kuwa na Programu ya kudhibiti vitendo vya kunakili kazi za watu yataongeza ubora wa Wanafunzi na Elimu wanazozipata.
Ameongeza kuwa pamoja na kazi hizo pia wanawafundisha jimsi ya kuandaa mitaala ambayo inaendana na viwango vya TCU kwa kuzingatia mahitaji ya wahitaji.
Dkt. Rwegasira amesema wakati wa kipindi cha Ugonjwa wa COVID 19 walikutana na changamoto ambazo ziliwafanya kutafuta mbinu mbadala za kutoa Elimu ya masafa na hii ilionekana ni nyenzo muhimu ambayo pia itasaidia Chuo kuongeza idadi ya wanafunzi kwa ngazi mbalimbali popote walipo kwa kuwapunguzia gharama.
Soma zaidi bofya hapa chini