Katika kuhakikisha huduma ya umeme inafika vijiji vyote nchini Serikali kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) imetenga kiasi cha sh. tirioni moja ili wananchi waweze kupata huduma hiyo.
Akizungumza wakati wa kukagua miradi ya umeme vijiji Kamishna Msaidizi wa Umeme kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Inocent Luoga amesema huduma hiyo pia itawafikia wananchi katika vitongoji vilivyopo kwenye vijiji 85 vya Mkoa wa Morogoro.
Katika bajeti hiyo Mkoa wa Morogoro umetengewa zaidi ya shilingi bilioni 42 kwa ajili ya huduma hiyo ya umeme kwenye vijijini 85 ambavyo vimeshafikiwa na REA kati ya vijiji vyote 165 ambavyo vinatarajiwa kufikiwa ifikapo mwezi Juni mwakani.
Sauti ya Mhandisi Inocent Makoye
Kwa upande wake Mhandisi Gasper Lyimo kutoka Kampuni ya State Grid inayojenga umeme vijijini katika mkoa wa Morogoro amewahakikishia wananchi wa Kijiji cha Vidunda kuwa mradi huo utakamilika kwa wakati
Sauti ya Mhandisi Gazepre Lyimo.
Nao wananchi wa Kata hiyo akiwemo Bi Marietha Makseyo na Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bw. Lazari Kiboga wamepongeza hatua hiyo kwa kuwa itasaidia kuleta maendeleo katika kijiji hicho
Sauti ya Bi Marietha Makseyo