Na.Vedasto George.
Wanawake wajasiriamali mkoani Morogoro wamesema licha ya mafanikio waliyonayo bado wanakabiliwa na changamoto mabalimbali ikiwemo mikopo isiyokidhi maitaji.
Wakizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika kimkoa Kijiji cha Changalawe wilayani Mvomero mkoani Morogoro wamesema mikopo midogo isiyo kidhi maitaji imekuwa changamoto katika kufikia malengo yao ya kibiashara.
Akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mkuu wa Wilaya ya Mvomero MOHAMED UTALI amesema Serikali inaendelea kufanyajitiada mbalimbali ikiwemo kutoa mikopo yenye riba nafuu itakayowawezesha wanawake kujiendeleze zaidi katika biashara.
Aidha Utali amesema serikali imeandaa mpango kazi wa kitaifa utakaosaidia kupunguza ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto wa mwaka 2017/2018 hadi mwaka 2020/2022 ambao unamikakati mbalimbali ikiwemo ya kuimalisha Uchumi wa Kaya na kuimalisha malezi na mahusiano katika ngazi ya familia.
Awali akimkaribisha mgeni rasimi Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro sehemu ya mipango na uratibu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Anza Hammed Ndosa amesema maadhimisho hayo ufanyika ili kuimarisha usawa wa kijinsia ikiwemo vyombo vya kutoa maamuzi.
Siku ya wanawake duniani mkoani Morogoro imepambwa na taasisi mbalimbali , ikiwemo wanawake Wahandisi wa Kampuni ya Afriqeu Power and Maintanance inayofanya matengeneo ya umeme bila kuzima huku yakiwa na kaulimbiu isemayo kizazi cha usawa kwa maendeleo ya Tanzania ya sasa na baadae.
Maadhimisho Hayo yalitanguliwa na utoaji wa zawadi kwa wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
Katika video bofya hapa chini