Na: Ayub Mwigune
Serikali imesema kuwa imeendelea kuweka jitihada mbalimbali katika kuhakikisha inakabiliana na athari za uharibifu wa hewa ukaa ikiwemo kuanzisha mabasi ya mwendokasi, treni ya mwendo kasi pamoja na miradi ya ujenzi wa reli yaani SGR pamoja na Stieglers Gorge.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu wakati akiwa katika ziara ya kutembelea Kituo cha Kuratibu Hewa Ukaa nchini Tanzania (NCMC) kilichopo Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA mkoani Morogoro.
Mhe. Zungu amesema athari kubwa ya mazingira nchini inatokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu lakini pamoja na kuwa na changamato za athari za hewa ya ukaa serikali imefanya jitahada mbalimbali ili kukabiliana na tatizo hilo ambapo imeleta mabasi ya mwendo kasi, treni ya mwendokasi na Mradi wa Stieglers Gorge huku akiwaomba wananchi kuchukua hatua ya ziada katika kuhakikisha wanapambana na uharibifu wa hewa ukaa nchini kwa kutumia nishati mbadala
Kuhusu Kituo cha Kuratibu Hewa ya Ukaa nchini Tanzania (NCMC) amepongeza namna amabavyo kimekuwa kikifanya kazi nchini kama kuzalisha takwimu ambazo zinasaidia Taifa katika majukumu yake ya kutoa ripoti inayohusu uzalishaji wa gesi joto na kueleza kwamba serikali ipo bega kwa bega na kituo hicho huku akiahidi kubeba changamoto za kituo hicho na kwenda kuzifanyia kazi
Kwa upande wake Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA (Taaluma) Prof. Peter Gillah akimuwakilisha Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof.Raphael Chibunda amesema Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kimefurahishwa na ujio wa Waziri wa Mazingira na Muungano na kuweza kujionea kituo cha kuratibu hewa ya ukaa NCMC huku chuo kikiahidi kuzidi kuonesha ushirikiano katika kukiboresha kituo hicho.
Naye Mratibu wa Kituo cha Kuratibu Hewa ya Ukaa Tanzania Prof. Eliakimu Zahabu amesema takwimu zinazozalishwa na kituo cha hicho zinatumika katika matumizi mbalimbali na kuweza kuwasaidia wananchi vilevile kituo hicho kimekuwa kikitoa mafunzo yanayohusiana na mabadiliko ya nchi katika maeneo mbalimbali nchini huku akimshukuru waziri kwa ujio wake katika kituo
Amesema ni wakati wa kukaa pamoja na kujadiliana kuhusu mabadiliko ya tabia nchi ili kuweza kuona athari za mabdiliko hayo na kuyakabiri.
KATIKA VIDEO BOFYAN HAPA CHINI