Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dr. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Bakari Msulwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro mkoani Morogoro.
Uteuzi huo umefanywa jumapili june 21, 2020 ambapo Bwana Msulwa anachukua nafasi ya Bi.Regina Chonjo ambaye amestaafu.
Kabla ya uteuzi huo, Bwana Msulwa alikuwa Afisa Muandamizi na Mtangazaji wa Shirika la Habari Tanzania TBC,
wakati huo huo Mhe. Rais Magufuli amemteua Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Edward Jotham Balele kuwa Mkuu wa Wilaya ya Monduli mkoani Arusha.
Bwana Balele amechukua nafasi ya Bwana Iddi Kimanta ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kabla ya uteuzi huo Balele alikuwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Wateule hao wanatakiwa kuwepo Ikulu Jijini Dar es Salaam juni 22, 2020 saa mbili na nusu asubuhi.