Na Gladness Mafuru
Imeelezwa kuwa mfumo wa Afya Data hivi sasa umeanza kutumiwa na nchi jirani kama Mozambique wakishirikiana na Wakfu wa Utafiti na Udhibiti wa Magonjwa Ambukizi ya afya moja wa SACIDS kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA.
Picha kutoka Maktaba |
Sauti ya Afisa Mawasiliano wa SACIDS Yunus Karsan
Hayo yameelezwa na Afisa Mawasiliano wa SACIDS Yunus Karsan April 28,2021 wakati akizungumza na SUAMEDIA ofisini kwake.
Karsan amesema hivi sasa tayari timu ya SACIDS kutoka SUA ipo Mozambique kwa ajili ya kutoa mafunzo ya namna ya kutumia mfumo wa Afya data katika kukusanya taarifa za magonjwa kutoka kwenye ngazi mbalimbali ya jamii kwa wanyama pia binadamu.
Ameongeza kuwa mfumo huu wa Afya data una wigo mpana wa kutumika na nchi zingine ulimwenguni kutokana na kuwa unaweza kubadili lugha kutokana na mahitaji ya eneo husika.
Aidha ametoa wito kwa wanafunzi wa SUA kwa ngazi za Uzamili na Uzamivu kujitokeza kwenye nafasi za kwenda kusoma nje ya nchi pamoja na kufanya tafiti hizo katika vyuo washirika kama vile NSG iliyopo South Afrika, Uingereza na Korea.