Na; MOHAMEDI TWAHA
Taasisi ya ASA ambayo inajihusisha na maswala ya kusambaza mbegu imewataka wakulima kununua mbegu zenye ubora ulio thibitishwa na watalamu iliwaweze kuepukana na tatizo la kupata mazao machache au kukosa kabisa .
Hayo yameelezwa na Emanuel Woga Mwesa meneja wa masoko kutoka ASA katika maonyesho ya hayati Edward Molinge Sokoine yanayo endelea katika viwanja vya sua kampasi kubwa.
Amesema wakulima wanatakiwa kupanda mbegu kutokana na sehemu walizopo kwani kuna maeneo ambayo hayana mvuanyingi hivo wanatakiwa kupanda mbegu ambazo hazi hitaji maji mengi na kuna maeneo ambayo yana mvuanyingi hivo wanatakiwa kupanda mbegu ambazo zinahitaji maji mengi.
Woga Mwesa amesema kuwa wakulima wanatakiwa kuepuka kurudia mbegu kwasababu husababisha kupata mazao machache na kadri wanavo rudia mbegu inapungua ubora na inaweza kufika sehemu asipate mazao kabisa pia husababisha magonjwa kwa mmea pale mbeguinapo isha ubora wake.
Pia amesema ASA wanatoa mbegu ambazo zinaubora mkubwa na dawa ambayo inasaidia mbegu isiharibiwe na wadudu haribifu na kufanya mmea utakao ota kuwa na rutuba.
Hatahivyo amesema kuwa wanatoa elimu kwa wakulima na sekta bnafsi kutambua mbegu zenye ubora na jinsi yakuhudumia mazao yao mpakapale yatakapo komaa ilikuwasaidia wakulima kupata mazao mengi na yenye ubora pia amewataka wakulima wapambane nakilimo chenye tija.