Rais Magufuli amewasimamisha kazi Waandisi 12 wa Tanroads Mkoa wa Morogoro kutokana na uzembe wa kukatika kwa daraja la kiegea katika barabara ya Morogoro/ Dodoma
Pia ametoa onyo kali kwa Waziri wa Ujenzi Mhandisi Isack Kamwelwe, Mtendaji Mkuu wa Tanroads pamoja baadhi ya waandisi kwa kushindwa kusimamia kikamilifu ujenzi wa daraja hilo lilipobomoka march 3 na kusabisha kukatika kwa mawasiliano baina ya Dodoma na Morogoro.
Sauti ya Mhe.Magufuli
Aidha Rais Magufuli ameagiza Meneja wote wa Tanroads mikoa wahakikishe wanasimamia vyema madaraja na barabara zote nchini endapo itatokea kukatika kwa daraja meneja husika aandikiwe barua ya kufukuzwa kazi
Kabla ya kufika mkoani Morogoro Rais Magufuli alitembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja la juu eneo la Ubungo linalounganisha barabara za Morogoro, Sam Nujoma na Mandela jijini Dar- es- salaam .
Sauti ya Mhe.Magufuli
WAKATI huo huo Waziri Kamwelwe amemuomba radhi Rais Magufuli kwa uzembe uliotokea katika daraja hilo na kukiri kwamba alitakiwa kumfukuza kazi mhandisi wa awamu ya kwanza alipowasili mkoani humo