Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametangaza kuwepo wagonjwa wengine wawili wa virusi vya Corona nchini Tanzania, ambao mmoja ni raia wa Marekani aliyepo jijini Dar es Salaam na raia wa Ujerumani aliyepo visiwani Zanzibar.Jumla ya waathirika wa virusi hivyo nchini wamefikia watatu“Tayari wagonjwa wawili wamepatikana wa maambukizi ya virusi vya Corona, mmoja kutoka Zanzibar, sampuli zake zililetwa maabara kuu yeye ni Mjerumani (24), yuko kwenye uangalizi, hapa Dar es Salaam tuna Mmarekani (61), na tutaendelea kuwahifadhi hawa hadi tukapojiridhisha tatizo limekwisha basi tutaweza kuwaondoa,” amesea Waziri Mkuu.
Pia amesitisha masomo kwa vyuo vikuu na vya kati nchini kuanzia leo March 18, 2020 ili kukabiliana na Virusi vya Corona
Source:
MPEKUZI
Via:
SUAMEDIA