Na : Kalokola Aporinary
Kutokana na taarifa zisizo rasmi juu uwepo wa wagonjwa wa Corona ndani ya Mkoa wa Morogoro, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare ameonya kwa kuwataka watu wanaosambaza taarifa za ugonjwa huo kuacha mara moja.
Akizungumza na waandishi wa habari katika kikao maalumu cha mwelekeo wa ugonjwa huo ndani mkoa wa Morogoro, Loata amekanusha juu ya taarifa hizo za upotoshaji kwa jamii na kuwataka wananchi na vyombo vya habari vinavyosambaza taarifa za uongo viache mara moja.
Amesema awali kuliwa na taarifa za watu waliodhaniwa kuwa na maambukizi ya virusi hivyo vya Corona, lakini baada kufanyiwa uchunguzi wa vipimo wamethibitika kutokuwa na maambukizi ya virusi hivyo vya Corona ambapo pia Mganga Mkuu wa mkoa Dkt Ukio Kusirye amesema Morogoro hakuna mgonjwa
Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare
Aidha mkuu wa Mkoa Loata, amewataka wazazi na walezi wa watoto kuwa makini katika kipindi hiki cha uwepo wa ugonjwa huo na Serikali ikiwa imezifunga shule zote ili kuepuka maambuzi ya virusi vya Corona.