Shirika la Hifadhi za Taifa na Wanyama pori (TANAPA) limesema lipo kwenye mpango wa kuongeza ndege mbili za kufanyia dolia ili kuimalisha ulizi katika hifadhi ikiwa ni njia moja wapo itakayowezesha kupambana na ujangili wa wanyamapori.
Akizungumza katika kikao kazi cha siku tatu cha Wadau wa Uhifadhi Hifdhi ya Taifa ya Nyerere Mkoani Morogoro Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, Dkt Allan Kijazi amesema TANAPA tayali imeisha weka mikakati endelevu ya kuhakikisha inadhibiti vitendo vya kijangili katika hifadhi za Wanyamapori na kuongeza kuwa ndege hizo zitasaidia kufika katika maeneo ambayo askari wa wamyamapori awawezi kufika kwa miguu.
Kwaupande wake Kamishna wa Uhifadhi TANAPA Kanda ya Mashariki Asteria Ndaga amesema wameaza kuimalisha vikundi vya ulinzi shirikishi katika hifadhi, huku akiongeza kuwa vikundi hivyo vimekuwa na mchango mkubwa katika kuimalisha ulinzi ikiwemo kuwafichua watu wanaojiusisha na vitendo vya ujangili.
Katika hatua nyingine Mwakilishi wa Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) Zahoro Kimwaga amebainisha kuwa kitendo cha kupandishwa hadhi sehemu ya poli la akiba la Selous kuwa Hifadhi ya Taifa ya Nyerere ni jambo jema na kusema Taasisi hizo mbili TAWA na TANAPA zinapaswa kushirikiana katika kuendesha hifadhi hiyo.