SUAMEDIA
No Result
View All Result
  • MWANZO
  • HABARI
    • All
    • Kimataifa
    • Kitaifa
    Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo chapongezwa kwa ubunifu katika Kilimo

    Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo chapongezwa kwa ubunifu katika Kilimo

    Human Rights Watch yahimiza uchunguzi wa kuaminika kuhusu miili iliyokutwa mtoni DRC

    Mubashara: Asubuhi hii: Mwili wa Hayati Mkapa kuelekea uwanja wa Uhuru

    LIVE: Mwili wa Rais Mkapa unaagwa Uwanja wa Uhuru, Mkewe aishiwa nguvu, Magufuli, majonzi yatawala

    BOOK OF THE WEEK- “Increasing Production from the Land: A Source Book on Agriculture for Teachers and Students in East Africa” 

    Mubashara:Kinachoendelea msibani kwa Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa muda huu

    Nafasi za Kazi katika Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa

    Tume ya Uchaguzi yabadili majina ya Majimbo matatu, yatangaza Tarehe ya Kutoa Fomu

    Rais Mkapa (Kuzaliwa, Elimu, Uongozi na Urais)

    • Kitaifa
    • Kimataifa
    • MAGAZETI
  • MAKALA
    • All
    • Hifadhi, Utalii na Mazingira
    • Kilimo
    • Ufugaji na Uvuvi

    VIDEO: SUA imeendeleza mkakati wa kuhakikisha wadau wa Elimu wanafikiwa kwa njia ya Elimu Masafa

    Video: Kilimo cha mbogamboga kwa kutumia viroba

    Naibu Waziri wa Ardhi Dkt. Mabula aipongeza Wizara Ya Ardhi kuwezesha Nchi kufikia Uchumi Wa Kati

    Serikali yazindua Chanjo za Kimkakati 13 za Mifugo, Waziri Mpina awaweka kitanzini Wakurugenzi

    Bupilipili: SUA inafanya mambo yake kwa vitendo ikiwa ni pamoja na utalii

    VIDEO: Katavi Mkoa wa Kilimo na Utalii unaotendea haki kasi ya maendeleo ya Serikali ya Awamu ya Tano

    Vyuo vya Kilimo nchini vyatakiwa kujiimarisha kimapato

    • Kilimo
    • Hifadhi, Utalii na Mazingira
    • Ufugaji na Uvuvi
  • TAFITI
  • MICHEZO & BURUDANI
  • 101.1 SUA FM
  • SUA TV
  • SUAMEDIA BLOG
SUBSCRIBE YOUTUBE

Home Movie

Nchiza SADC zatakiwa kupambana na Ugaidi na Utakatishaji Fedha Haramu

by Tatyana Celestine
July 14, 2020
min read3 min
1

RELATED POSTS

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo chapongezwa kwa ubunifu katika Kilimo

Human Rights Watch yahimiza uchunguzi wa kuaminika kuhusu miili iliyokutwa mtoni DRC

Mubashara: Asubuhi hii: Mwili wa Hayati Mkapa kuelekea uwanja wa Uhuru

Buy JNews
ADVERTISEMENT
Na Farida Ramadhani, Dar es Salaam
Nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) zimeshauriwa kuunganisha nguvu zao kupambana na changamoto ya utakatishaji fedha haramu na ufadhili wa makundi ya kigaidi zinazotishia usalama na kuharibu uchumi wa nchi hizo  .
Ushauri huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mwenyekiti wa Maafisa Wandamizi wa HAZINA wa SADC, Bw. Doto James wakati akifungua Kikao cha Maafisa Waandamizi (Makatibu Wakuu) wa HAZINA na Benki Kuu wa nchi wanachama wa SADC uliofanyika kwa njia ya mtandao kutokea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNCC) jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika kikao hicho, Bw. James ambaye ni Mwenyekiti wa kikao hicho kitakachofanyika kwa siku mbili, alisema kuwa changamoto hiyo imesababisha baadhi ya nchi wanachama kuingia katika orodha ya nchi zilizo kwenye athari ya kuingia kwenye vikwazo vya kimataifa kwa kushindwa kutimiza vigezo na masharti ya Kikosi cha Masuala ya Fedha (Financial Action Task Force), hali iyonaweza kuathiri malengo ya jumuiya ya kuvutia uwekezaji.
Alisema licha ya kuwepo kwa changamoto hiyo na nyingine kadhaa za kijamii, kimazingira na kiuchumi Jumuiya hiyo imeendelea kutekeleza azma yake ya kufikia malengo ya maendeleo iliyojipangia kupitia Mkakati Elekezi wa Maendeleo wa SADC hali inayoashiria kuwa Jumuiya hiyo ni imara kutokana na kuwepo kwa sera nzuri na mifumo mizuri wa kitaasisi ndani ya Jumuiya hiyo.
“Pamoja na mafanikio ya kiuchumi yaliyopatikana kwa miaka ya hivi karibuni, baadhi ya nchi wanachama zimeendelea kukabiliana na changamoto nyingine katika sekta za uchumi ikiwemo ukuaji mdogo wa uchumi, kuongezeka kwa nakisi ya bajeti na hii changamoto mpya ya ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya corona”, alisema.
Bw. James alisema katika kikao hicho Makatibu Wakuu hao watajadili na kutoa mapendekezo ya ajenda mbalimbali za masuala ya fedha na uwekezaji kwenye nchi za SADC ikiwemo athari za Kiuchumi na Kijamii zinazotokana na mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 yatakayowasilishwa kwenye Mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Fedha na Uwekezaji na Magavana wa Benki Kuu wa SADC utakaofanyika tarehe 15 Julai, 2020
Alisema kuwa Kamati ya Mawaziri wa Fedha na Uwekezaji, pamoja na mambo mengine, wanajukumu la kusimamia itifaki ya Fedha na Uwekezaji katika Jumuiya ya SADC kwa lengo la kuhakikisha Sera na Maamuzi ya Baraza la Mawaziri wa SADC kwenye masuala yanaohusu Fedha na Uwekezaji vinatekelezwa.
“Ili kukabiliana na athari hizo, ni vema nchi wanachama kutumia mifumo ya kitaasisi katika kutafuta njia mbadala zenye ubunifu ili kuharakisha hatua za kuimarisha uchumi ndani ya jumuiya yetu, ni matumaini yangu kuwa kikao hiki ni njia muafaka katika kujadili changamoto za kiuchumi na kutoa mapendekezo ya kitaalam yatakayowasilishwa katika Mikutano ya Kamati ya Mawaziri wa Fedha na Uwekezaji na Magavana wa Benki Kuu kama ilivyoanishwa katika agenda za mikutano hiyo”, alisema Bw. James.
Alizitaja ajenda nyingine watakazo jadili na kutoa mapendekezo kuwa ni kupitia  taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Mkutano uliopita  wa Kamati ya Mawaziri wa Fedha na Uwekezaji uliofanyika Windhoek, Namibia mwezi Julai 2019, kupokea na kujadili taarifa ya hatua iliyofikiwa ya namna uendeshaji wa Mfuko wa Maendeleo wa Kikanda wa SADC (SADC Regional Development Fund) na kupokea taarifa ya utekelezaji wa Mfuko wa Maandalizi ya Miradi ya Maendeleo wa SADC (Project Preparation Development Facility).
Viongozi hao pia watajadili  na kupata taarifa ya hatua iliyofikiwa katika uanzishaji wa Mfuko Maalum wa Kugharamia Miradi ya Muundombinu ya Usafirishaji wa Nishati ya Umeme (Regional Transmission Infrastructure Financing Facility – RTIFF) inayofadhiliwa na Benki ya Dunia, kupitia taarifa ya maendeleo ya Sekta ya Fedha ya Magavana wa Benki Kuu nakupitia taarifa ya utekelezaji wa masuala ya udhibiti wa fedha haramu.
Mkutano  wa Kamati ya Mawaziri wa Fedha na Uwekezaji na Magavana wa Benki Kuu wa SADC unaondaliwa katika kikao hicho ulipangwa ufanyike kuanzia tarehe 13 hadi 17 Julai, 2020 lakini kutokana na mlipuko wa COVID-19, mkutano huu utafanyika kwa njia ya mtandao kama ilivyoelekezwa katika  Mkutano wa dharura wa Baraza la Mawaziri wa SADC uliofanyika tarehe 18 Machi 2020, Dar es Salaam.
Source: MPEKUZI
Via: SUAMEDIA
ShareTweetPin

Tatyana Celestine

Related Posts

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo chapongezwa kwa ubunifu katika Kilimo
Kilimo

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo chapongezwa kwa ubunifu katika Kilimo

September 16, 2020

Human Rights Watch yahimiza uchunguzi wa kuaminika kuhusu miili iliyokutwa mtoni DRC

August 13, 2020
Kitaifa

Mubashara: Asubuhi hii: Mwili wa Hayati Mkapa kuelekea uwanja wa Uhuru

September 16, 2020
Kitaifa

LIVE: Mwili wa Rais Mkapa unaagwa Uwanja wa Uhuru, Mkewe aishiwa nguvu, Magufuli, majonzi yatawala

September 16, 2020
Kilimo

BOOK OF THE WEEK- “Increasing Production from the Land: A Source Book on Agriculture for Teachers and Students in East Africa” 

September 16, 2020

Mubashara:Kinachoendelea msibani kwa Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa muda huu

July 24, 2020
Next Post

Habari Katika Magazeti ya Leo Jumatano July 15

SUA yaendeleza mkakati wa kufikisha Elimu kwa njia ya Masafa kwa Wadau wake

Comments 1

  1. Gertrude Maha says:
    2 months ago

    i like this well article

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published.

HABARI MPYA

  • Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo chapongezwa kwa ubunifu katika Kilimo
  • Habari katika Magazeti ya leo Jumatatu August 17
  • Habari katika Magazeti ya leo Ijumaa August 14
  • Human Rights Watch yahimiza uchunguzi wa kuaminika kuhusu miili iliyokutwa mtoni DRC
  • Mubashara: Asubuhi hii: Mwili wa Hayati Mkapa kuelekea uwanja wa Uhuru
  • MWANZO
  • HABARI
  • MAKALA
  • TAFITI
  • MICHEZO & BURUDANI
  • 101.1 SUA FM
  • SUA TV
  • SUAMEDIA BLOG

© 2020 Sokoine University of Agriculture Media, Tanzania