Bondia wa Kimataifa wa Tanzania Hassan Mwakinyo anatarajiwa kupanda ulingoni Agosti 14 mwaka huu kuwania ubingwa wa uzito wa SuperWeight wa WBF raundi 12 dhidi Bondia kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Tshibangu Kayembe katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Tangu mwaka huu uingie Bondia Mwakinyo hajawahi kushuka ulingoni ambapo mara mwisho pambano lake dhidi ya Mjerumani Jack Coulkey lililopangwa kufanyika mwezi Machi lilihairishwa kutokana na janga la virusi vya Corona.
Kuelekea pambano hilo Mwakinyo amewataka Watanzania kujitokeza kutoa hamasa ambapo maandalizi kwa upande wake amesema yanakwenda vizuri na kuahidi kutoa burudani kwa wapenda msumbwi.
Rekodi za mabondia wote wawili zinaonyesha kuwa Mwakinyo amepigana mapambano nane na kupoteza moja wakati Kayembe amepigana mapambano 12 akishinda tisa na kutoa sare mara tatu.