Na: Farida Mkongwe
Serikali ya mkoa wa Morogoro imekipongeza Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kwakuwa wabunifu katika masuala yanayohusu kilimo hali inayosaidia kutatua changamoto za wakulima nchini.
Mhandisi Emmanuel Kalobelowakati akizungumza kwenye sherehe za kumpongeza na kumtakia heri aliyekuwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Taaluma) Prof. Peter Gillah ilizofanyika katika ukumbi wa Multipurpose uliopo Kampasi Kuu ya SUA mjini Morogoro.
Mhandisi Kalobelo amesema “SUA hakuna mfano wenu, sisi kama serikali tunajivunia sana uwepo wa chuo hiki hapa mkoani Morogoro, mmekuwa mfano wa kuigwa mnatumia ubunifu wenu kutafuta changamoto zinazowakabili wakulima na kisha mnatafuta ufumbuzi, kwa hilo nawapongezeni”.
“Ubunifu wenu ni katika taaluma, sisi ambao tupo serikali ni
wadau wenu wa bidhaa mnazozalisha ambazo ni wanafunzi, sijawahi kunung’unikia wanafunzi au wafanyakazi anaotoka SUA, ni wazi kuwa vijana wenu mnawapika vizuri ili ni lazima mliendeleze”, alisisitiza Katibu Tawala huyo wa mkoa wa Morogoro.
Amesema kuwa serikali inahitaji sana kutumia elimu na kutoa
wito kwa SUA kuendelea kutoa elimu kwa vitendo ili elimu hiyo iweze kuwasaidia wananchi na hasa wakulima huku akihimiza mahusiano mazuri baina ya SUA na taasisi nyingine za serikali.
“ Tungetaka kuona na tunapenda kwa kweli yawepo mahusiano ambayo yatatatua changamoto zilizopo, inashangaza kuona halmashauri zinakuwa na changamoto ambazo nyie SUA mnayo majibu ya changamoto hizo”, alisema.