Kozi mpya ya Misitu Biashara, Ujasiriamali na Masoko itawasaidia wahitimu na wakulima

Wakulima wa miti fuateni njia bora za kilimo cha miti

 

Prof. Jumanne Abdallah akitoa ufafanuzi katika warsha ya kujadili kozi mpya SUA 

 

Na Gerald Lwomile, Dar es Salaam

Mkuu wa Idara ya Uchumi Misitu na Mazingira Prof. Jumanne  Abdallah   amesema kozi mpya ya Misitu Biashara, Ujasiriamali na Masoko inayotarajiwa kuanzishwa SUA inaweza kufundishwa katika ngazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Diploma, Shahada ya Kwanza na hata Shahada za Juu kama ambavyo wadau mbalimbali wameshauri

Prof. Abdallah amesema hayo katika warsha ya siku moja ya kujadili namna bora ya kuendesha kozi hiyo na iwekwe katika ngazi ipi warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni

Amesema wao kama Idara chini ya Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii iliyopendekeza kozi hiyo ni muhimu wakafuata maoni ili kulisaidia Taifa, wahitimu na wakulima wa zao la miti nchini

Katika hatua nyingine wakulima wa miti nchini wametakiwa kujua taratibu za kupanda miti hasa kwa kuzingatia upandaji wa awamu ili kuwa uvunaji endelevu  ambao utawasaidia pia kupata kipato kila wakati na hivyo kuwaletea  matokea mazuri  katika kilimo Biashara cha miti

Hayo yamesemwa na Mhadhiri Mwandamizi kutoka Ndaki ya Misitu, Wanyapori na Utalii Prof. Felister Mombo wakati akitoa ufafanuzi wa kozi mpya ambayo inatarajiwa kuanzishwa SUA itakayoandaa wahitimu  katika kozi ya Misitu Biashara, Ujasiriamali na Masoko

Prof. Mombo amesema wakati mwingine inashangaza kuona mtu ana shamba la ukubwa wa ekari kadhaa na anaamua kulipanda miti lote na kusubiri hadi miaka kadhaa kabla ya kuvuna wakati angeweza kupanda shamba hilo kwa awamu huku akiacha eneo jingine litumike kwa uzalishaji wa mazao ya muda mfupi

Amesema haya ni baadhi ya mambo ambayo mkulima akifundishwa yatamsaidia kuhakikisha anakuwa na kipato kwa muda wote.

Warsha hiyo ya siku moja ambayo imefanyika jiji Dar es Salaam ilikuwa na lengo la kutaka kupata maoni ya wadau kuhusu kozi hiyo mpya.

Related Posts

Next Post

Discussion about this post

RECOMMENDED