NA.AYOUB MWIGUNE
LIGI Kuu Tanzania Bara itaendelea leo Februari,5,2020 kwa timu 14 zitakuwa uwanjani kwa kutafuta alama tatu katika viwanja tofauti
Ratiba inaonyesha kwamba klabu ya Namungo itacheza dhidi ya Alliance, katika uwanja wa Majaliwa. huku Ndanda wakivaana na Mbao uwanja Nangwanda.
klabu ya Mbeya City wataikaribisha KMCkatika dimba la Samora. Nao Kagera Sugar watajinoa mbele ya Mwadui huko Kaitaba mkoani kagera
.
Ruvushooting watakuwa na kibarua kigumu mbele ya V Mtibwa Sugar uwanja wa Mabatini
Azam wao watamenyana na Prisonsuwanja Taifa, Saa 10:00 Jioni Yanga wataikaribisha Lipuli kutoka Iringa katika uwanja wa Taifa, Saa 1:00 Usiku.