Na.Vedasto George.
Chuo Kikuu Cha Sokoine cha Kilimo SUA kwa kushirikiana na vyuo vikuu viwili Afrika Mashariki ambavyo ni Kenya,Uganda na chuo cha Michigan State University cha nchini Marekani vimeanzisha mpango wa kuendeleza vijana wajasiriamali wavumbuzi lengo likiwa ni kuwajegea uwezo wa kujiajiri katika biashara.
Akizungumza katika semina ya siku moja ya kuendeleza vijana wajasiriamali wavumbuzi hususani mabinti Mratibu wa mpango huo nchini Tanzania ambaye pia ni Mratibu wa kituo cha maswala ya Taaluma za Jinsia SUA kutoka katika Daki ya Sayansi za Jamii na Insia Profesa Mshiriki John Jecknoiah amesema, mpango huo unalenga wajasiriamali wote vijana wakike na wakiume, na kuongeza kuwa mpaka sasa wajasiriamali takribani kumi na sita kutoka tanzania wamekwisha nufaika.
Aidha Prof. Jecknoiah amesema kuwa kwa Tanzania vijana ndo nguvu kazi ya Taifa huku akiongeza kuwa takwimu zinaonesha kuwa vijana wa kike ndiyo wanaokumbana na vikwazo vikubwa katika kutafuta ajira na kuwaomba vijana kubadili mtazamo wa kusubiri kuajiriwa hivyo amewataka kuweka mipango ya kujiajiri wenyewe.
Awali akifungua semina hiyo Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Jamii na Insia Dr.Samweli Kabote amesema ushirikiano wa vyuo hiyo unalenga kujenga uwezo wa wajasiriamali huku akisema SUA imekuwa na ushirikano mzuri na vyuo vingine hususani chuo cha Michigan State University cha nchini Marekani.
Bi. Theresia Jacob ni nimiongoni mwa wasichana walionufaika na mpango wa kuendeleza vijana wajasiriamali wavumbuzi nchini ameeleza namna alivyo weza kujiunga na mpango huo huku akiongeza kuwa tangu ajiunge ameweza kufanya kilimo,na kufanya Biashara mbambali.