Kugunduliwa kwa Mafuta na Gesi katika baadhi ya nchi za Afrika kumeweza kuokoa fedha nyingi ambazo zingetumika kununua nishati nje kwa matumizi mbalimbali ya maendeleo.
Kwa kipindi cha miaka 15, toka Tanzania ilipoanza kuzalisha na kusambaza gesi, imeokoa kiasi cha shilingi Trilioni 30, ambazo zingetumika kuagiza mafuta nje kwa ajili ya kuzalisha umeme na uendeshaji wa viwanda.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC James Mataragio, takriban asilimia 60 ya umeme unaozalishwa nchini unatumia gesi asilia, huku nishati hiyo pia ikitumika viwandani mbali na kutumika kuendesha magari katika siku za hivi karibuni.
Zaidi tembelea BBC SWAHILI