SUA na Chuo Kikuu cha Greenwich cha Uingereza zaingia mkataba wa makubaliano ya ushirikiano

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, SUA kimeingia mkataba wa makubaliano ya ushirikiano (MoU) na Chuo Kikuu cha Greenwich cha Uingereza kupitia programu ya Mpango wa Usalama wa Chakula na Lishe (FaNSI) ya Taasisi ya Maliasili (NRI)

Makubaliano hayo yaliyofanyika Kampasi Kuu ya Chuo Kikuu cha Sokoine chaKilimo tarehe 16 Oktoba 2019 yalitanguliwa na uwasilishwaji wa taarifa na historiafupi za vyuo hivyo viwili.Lengo la makubaliano hayo ni kushirikiana katika Nyanja mbalimbali ikiwemokatika Shahada za Uzamivu na kubadilishana uzoefu wa namna ya kuandikamaandiko ya mapendekezo huku Kituo cha Kudhibiti wa Viumbe hai waharibifukutoka SUA kikiwa moja ya wadau pekee wa program hiyo katika Nchi za kusiniwa Jangwa la Sahara.Kupitia makubaliano hayo Mwanataaluma mmoja wa SUA amefanikiwa kupataufadhili wa shahada ya uzamivu kwenda kusoma na kujifunza katika Chuo Kikuucha Greenwich Januari 2020.
Mkurugenzi wa Kituo cha Kudhibiti wa Viumbe hai waharibifu, Dkt. LadislausMnyone amekipongeza Chuo kikuu hicho cha Greenwich kwa kufanikisha swalahilo ambalo litaleta tija baina ya vyuo vyote viwili.Dkt. Mnyone amewashauri wanafunzi kuchangamkia fursa hiyo hasa kwenyeupande wa tafiti ambazo zinazoweza kutatua changamoto mbalimbali Tanzania naduniani kwa ujumla.NRI ni taasisi iliyobobea kwenye tafiti za maendeleo ya kijamii kama Chakula,Kilimo, Mazingira na Maisha Endelevu ambayo inasimamia programu ya Mpangowa Usalama wa Chakula na Lishe (FaNSI) ili kutatua changamoto zinazolikumbabara la Afrika hasa kwenye upatikanaji wa mlo kamili.Chuo Kikuu cha Greenwich kupitia FaNSI kinafanya kazi na taasisi mbalimbalibarani Afrika ambapo Chuo Kikuu cha Sokine cha Kilimo, SUA ikiwa ni moja yataasisi hizo kwa sasa.

Related Posts