Daraja linalounganisha njia  ya kwenda Hospitali ya Rufaa ya Morogoro na Makao Makuu ya Mkoa labomoka

Na: Kalokola Aporinary

Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini huku zikileta athari za uharibifu wa miundombinu wakazi wa Mtaa wa Nguzo manispaa ya Morogoro wamelalamikia changamoto ya kubomoka kwa daraja linalounganisha njia  ya kwenda Hospitali ya Rufaa ya Morogoro na Makao Makuu ya Mkoa.

 

Wakizungumza katika tukio hilo na kushuhudia athari zilizojitokeza kufuatia kubomoka kwa daraja linalodaiwa kuathirika kufuatia kingo zake kujaa uchafu hali iliyopelekea maji kuharibu vibaya daraja hilo, wakazi wa mtaa huo wameeleza namna wanavyopata changamoto.

 

Aidha Mwenyekiti wa Mtaa huo ameeleza hatua alizochukua mara baada ya kubainika kwa kuwepo kero hiyo huku Meneja wa Tarura Mkoa wa Morogoro James Mnene akieleza mipango iliyopo katika kuhakikisha miundombinu yote iliyoharibika wakati huu wa mvua inafanyiwa marekebisho likiwemo daraja hilo 

 

Related Posts

Next Post

Discussion about this post

RECOMMENDED