Wadau sekta ya maziwa toeni mapendekezo kuboresha sekta hiyo

Yatasaidia kuongeza tija

Na Calvin Gwabara    

Morogoro           

Wadau wa sekta ndogo ya maziwa nchini wametakiwa kutoa mapendekezo ambayo yatasaidia kuifanya sekta hiyo iongeze tija kwa wadau wote kwenye nyororo wa thamani na kuongeza pato la taifa.

Mkurugenzi wa Mipango na Sera wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Zepania akizungumza na wadau wa sekta ya maziwa (Picha zote na Calvin Gwabara)

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Mipango na Sera wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Amosy Zephania wakati akifungua mkutano wa wadau wa sekta ya maziwa uliokuwa unajadili matokeo ya utafiti wa gharama za uzalishaji maziwa nchini.

Amesema kuwa wizara inatumia matokeo ya tafiti katika kutekeleza mipango mbalimbali ya kuendeleza sekta ya mifugo na uvuvi hivyo matokeo ya utafiti huo ambao umeletwa mbele ya wadau kujadiliwa na kutoa mapendekezo yao utasaidia wizara kujipanga ili kuongeza tija.

“ Napongeza kazi kubwa iliyofanywa na watafiti hawa pamoja na wadau waliosaidia kufanikisha utafiti huu mzuri na kuandaa mkutano huu muhimu wa wadau wa mnyororo wa thamani, niwaombe mtoe mapendekezo mazuri ili kuisaidia sekta yetu ya maziwa” Amesema Bw. Zephania.

Ameishukuru ANSAF kwa jitihada zake mbalimbali ambazo imekuwa ikizifanya katika kusaidia kuboresha sera na sheria zilizopo na kupatikana sera mpya na sheria ambazo zinaleta tija katika wizara ya mifugo na uvuvi lakini pia kwa wafugaji na sekta zingine.

Mkurugenzi huyo amewataka wadau wote kwenye mnyororo mzima wa thamani wa maziwa waliopo kwenye mkutano huo kujadili na kutoa mapendekezo yao kwa uhuru na kwa faida ya wadau wote na sio kuvutia upande mmoja na kuumiza wengine.

Akiwasilisha matokeo ya utafiti huo Mratibu wa dawati la sekta binafsi Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Steven Michael amesema utafiti huo uliwafikia wadau 80 katika nyororo wa thamani na kuzungumza nao kwa kina changamoto na faida na kupata mapendekezo yao.

Mratibu wa dawati la sekta binafsi Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Steven Michael akiwasilisha matokeo ya utafiti

Ameongeza kuwa pamoja na mambo mengi ambayo utafiti huu umeyabaini lakini swala la kuongeza uzalishaji kwa wafugaji kutasaidia kupunguza gharama za jumla kwa lita moja ya maziwa na hivyo kuongeza kipato cha mfugaji.

“Pamoja na Tanzania kushika nafasi ya pili kwa idadi ya mifugo barani afrika lakini fursa hiyo bado haijatumika vizuri na hivyo mchango wake katika pato la taifa kuwa ndogo kwani inachangia asilimia 1.2% kwenye GDP tofauti na majirani zetu ambao hawana mifugo mingi kama sisi” Amebainisha Bw. Michael

Pia amesema katika utafiti huo wamebaini kuwa uzalishaji mdogo wa maziwa bado umeendelea kuwa tatizo kubwa hasa kwa wafugaji wadogo ingawa sasa serikali imeipatia kipaumbele sekta hiyo hasa katika sera yake ya viwanda,Usalama wa chakula na lishe na Kipato.

Awali akizungumzia malengo ya mkutano huo wa wadau Meneja Ufundi kutoka Bodi ya Maziwa Deogratius Mlay ambaye alimuwakilisha Kaimu msajili wa bodi ya maziwa amesema sekta ya maziwa ina fursa nyingi lakini pia changamoto ambazo kwa ujumla utafiti huo umeziangalia kwa kina na kuja na mapendekezo.

“Tafiti ni kitu muhimu sana kwetu kama bodi ya maziwa lakini pia ni muhimu kwenye kila sekta maana kupitia utafiti ndipo mnapoweza kujua changamoto,faida na namna ya kukabiliana nazo ili kuongeza tija hivyo nasi tunafurahi kukamilisha utafiti huu ambao leo sasa tunauleta kwenu wadau mtusaidia kuuchambua na kutoa mapendekezo yenu pale ambapo mnaona pamesahaulika” Amesema bwana Mlay.

Meneja Ufundi kutoka Bodi ya Maziwa Deogratius Mlay akiongea kwenye mkutano wa wadau wa maziwa

Akitoa mapendekezo yake Prof. Lusato Kurwijila ambaye ni mtafiti aliyebobea kwenye sekta ya maziwa nchini kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA amesema unywaji mdogo wa maziwa nchini unatokana zalishaji mdogo wa maziwa kiasi kwamba watu wanakunywa yale ambayo wanaweza kuayapata lakini yakizalishwa mengi pia unywaji utaongezeka.

“ Lazima tuangalie changamoto za uzalishaji mdogo wa maziwa zi zipi ili tuzitafutie ufumbuzi na zikipata ufumbuzi na maziwa yakaongezeka nina uhakika kuwa unywaji wa maziwa nao utaongezeka na kufikia kile kinachopendekezwa na WHO” amesema Prof. Kurwijila.

 

Prof. Lusato Kurwijila ambaye ni mtafiti aliyebobea kwenye sekta ya maziwa nchini akichangia katika mkutano wa wadau wa sekta y maziwa

Kwa upande wake Bi. Rehema Mmari kutoa kampuni ya SHAMBANI MILK amesema wao kama wasindikaji wakubwa wanalipa kodi inayochangia maendeleo ya nchi tofauti  wale wasiosindika ambao hawalipi chochote lakini wanashindanishwa kwenye bei wakati wao hawasimamiwi na kuathiri upatikani wa maziwa kwa wasindikaji.

Asilimia 90 ya maziwa yanayozalishwa yanuzwa kiholela na hayaendi kwa wasindikaji na hivyo kuathiri upatikanaji wa maziwa kwa wasindikaji lakini wao wanauzaji wa kiholela wananunua kwa bei lakini hawasimamiwi kwakuwa hawaangalii hata ubora wa maziwa hivyo serikali kama kweli imeamua kuisimamia sekta basi wauzaji wa rejareja nao waangaliwe walipe kodi.” Alisema Mmari.

Related Posts

Next Post

Discussion about this post

RECOMMENDED